Posts

Mbunge Jimbo la Ubungo Chadema, John Mnyika:Hatua kuhusu matumizi ya dola milioni 164.6 za “mabomba ya mchina” na mikataba ya miradi ya sasa ya maji jijini Dar es salaam

Image
    Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini,John Mnyika ---    Tarehe 3 Januari 2013 kwa kutumia kifungu cha 10 cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge nimetaka Wizara ya Maji inipatie nakala ya ripoti ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotekelezwa kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 jijini Dar es salaam. Nimetaka ripoti hiyo ili kubaini matumizi ya dola milioni 164.6 zinazoelezwa kutumika katika mradi huo maarufu kama wa ‘mabomba ya mchina’ kwa kuwa mpaka sasa mwaka 2013 sehemu kubwa ya mabomba yaliyowekwa wakati wa mradi huo katika Jiji la Dar es salaam hayatoi maji huku kukiwa na upungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji, udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katika matumizi. Pamoja na kutaka ripoti ya utek...

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

Image
   Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha kwenye mkutano wa Chadema Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni akiwa ndani ya gari ya jeshi baada ya kutiwa nguvuni,   Picha juu alipopiga picha na Viongozi mbalimbali wa Chadema Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni. ---   Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari, ila aliwahi kuwa JKT na akaacha. Amekuwa ak...

Kipanya

Image

Mbunge wa Ubungo Chadema John Mnyika Akabidhi Zawadi Rasmi Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiriamali Jimbo la Ubungo

Image
Mshindi wa Tatu: Seif Juma (19) kutoka Goba Tsh 50,000/- Mshindi wa Kwanza: Joseph R. Shindo (22) kutoka Kata ya Kimara Tsh 200,000/- Mshindi wa Pili: Rehema A. Abdallah (25) kutoka Makurumla Tsh. 100,000/- Washiriki wote wa shindano, pamoja na waratibu na Mbunge wa Jimbo la Ubungo.Picha na Habari Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo -- Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa ushirikiano na shirika la Maendeleo Ubungo; Ubungo Development Initiative (UDI) waliendesha shindano la kuwainua wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwataka kuandaa mchanganuo namna gani watatumia Tsh 200,000/- katika kuanzisha au kuiendeleza biashara zako. Washindi waliopatikana ni;

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula:“Kwa kuwa tayari Rais ameshasema kuwa suala la gesi kubaki Kusini halikubaliki, wanaompinga ni waasi,”

Image
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula --- MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amesema viongozi wanaopinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wanafanya uasi na kuvunja nidhamu ya demokrasia.Mangula alitoa kauli hiyo jana alipokuwa anazungumzia kauli za makada wa CCM wanaompinga Rais Jakaya Kikwete kuhusu msimamo huo wa Serikali. “Kwa kuwa tayari Rais ameshasema kuwa suala la gesi  kubaki Kusini halikubaliki, wanaompinga ni waasi,” alisema. Ingawa Mangula hakuwataja makada hao, Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, Ali Chinkawene na Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji ni miongoni mwa makada waliopinga suala hilo waziwazi. Chinkawene alisema msimamo wa CCM Mkoa wa Mtwara, ni kuungana na wananchi kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam na kwamba Serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara. Mbunge Murji alikwenda mbali zaidi akisema yupo tayari ik...

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aogoza Mazishi ya Msanii wa Bongo Movie Juma Kilowoko (Sajuki)makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Leo

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki  wakati wa mazishi ya msanii huyo  leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.Picha na IKULU

HOJA YA HAJA YA MBUNGE WA KILWA KASKAZINI KUHUSU GESI ASILIA

Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini.  Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji. Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta.  Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni , nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri ...