MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula:“Kwa kuwa tayari Rais ameshasema kuwa suala la gesi kubaki Kusini halikubaliki, wanaompinga ni waasi,”

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula
---
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amesema viongozi
wanaopinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam
wanafanya uasi na kuvunja nidhamu ya demokrasia.Mangula alitoa kauli
hiyo jana alipokuwa anazungumzia kauli za makada wa CCM wanaompinga
Rais Jakaya Kikwete kuhusu msimamo huo wa Serikali.
“Kwa kuwa tayari Rais ameshasema kuwa suala la gesi kubaki Kusini halikubaliki, wanaompinga ni waasi,” alisema.
Ingawa Mangula hakuwataja makada hao, Mwenyekiti
wa CCM Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, Ali Chinkawene na Mbunge wa
Mtwara Mjini, Hasnain Murji ni miongoni mwa makada waliopinga suala hilo
waziwazi.
Chinkawene alisema msimamo wa CCM Mkoa wa Mtwara, ni kuungana na
wananchi kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam na kwamba
Serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara.
Mbunge
Murji alikwenda mbali zaidi akisema yupo
tayari ikibidi, kuvuliwa ubunge kwa kutetea masilahi ya Wanamtwara
kuliko kuona gesi hiyo ikisafirishwa kwenda Dar es Salaam.Mangula
alisema mtu mmojammoja, hawezi kutoa msimamo wake na kudai kuwa ni
msimamo wa chama.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........>>>>>>