Posts

MAJAMBAZI YAPORA RAIA WA UHOLANZI

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawasaka Watu wawili kwa tuhuma za   Unyang’anyi wa kutumia nguvu baada ya kuwatisha kwa   jambia wasichana wawili raia wa Uholanzi   na kisha   kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki mbili na sitini na nne elfu.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo lilitokea muda wa saa saba na dakika arobaini na tano mchana katika   eneo la area D Wilaya ya Dodoma Mjini,   Karibu na nyumba inayojengwa kwa ajili ya 0fisi na   Makazi ya Mh. Waziri   Mkuu   Bw. MIZENGO KAYANDA   PETER PINDA. Alitaja vitu vilivyoporwa katiika tukio hilo kuwa ni Kamera ya digitali aina ya Canon, Simu mbili za mkononi aina ya Nokia na Samsung, Begi la Mgongoni, Viatu vya wazi pea mbili (Sandal) Taulo la Hostel, Sketi, Wallet na Pesa za kitanzania shilingi 40,000/=. Aidha aliwataja Waathirika   wa Unyang’anyi huo kuwa ni wa LISA D/O LEMEN mwenye umri wa ...

MDENMARK ALETWA NCHINI

Image
KOCHA wa timu za Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 na 20 kutoka nchini Denmark atawasili nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza rasmi kazi ya kuzinoa timu hiyo. Kocha huyo mrithi wa Kim Poulsen aliyepewa jukumu la kuifundisha timu ya Taifa, Taifa Stars, baada ya aliyekuwa Mdemark mwenza Jan Poulsen kumaliza muda wake. Rais wa Shirikisho la soka Tanzania a (TFF) Leogegar Tenga, alisema kuwa tayari imeshafanya mazungumzo na makocha zaidi ya watatu kutoka nchini humo. Alisema kuwa timu ya Taifa Stars ipo chini ya kocha kutoka Denmark ndiyo maana wameamua kumtafutakocha mwingine kutoka nchini humo. Tenga alisema hata kipindi cha kocha wa timu ya Taifa akiwa Mbrazil Marcio Maximo, alikuwa akileta makocha kutoka nchini humo. "Tumeongea na Kim ametupa majina ya makocha watatu ambao tumeshaangalia na kuona kuna ambaye atakuja nchini kufanya kazi nasi....na hata alivyokuwa Maximo alikuwa akituambia makocha gani wanafaa nasi tuliamua kuwatafuta"alisema Tenga.

BASATA

Image
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya kuhimili ushindani wa kimataifa kutokana na ujio wa mfumo wa digitali ambao utazifanya kazi zao kuonekana kimataifa. Wito huo umetolewa wiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Ghonche Materego wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa uliohusu Teknolojia ya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya Sanaa uliochokozwa na Mhandisi Joel Chacha kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra). Alisema kuwa, mfumo wa digitali utaruhusu uwepo wa vituo vingi vya redio na runinga ambavyo vitakuwa na masafa ya kimataifa hivyo ni wazi wasanii wanatakiwa kujipanga katika kuandaa maudhui bora, ya kutosha na yenye mvuto kwa ajili ya kukidhi ongezeko hilo na zaidi ushindani wa kimataifa. “Wasanii tujipange, fursa zinazokuja ni nyingi mno, zinahitaji maudhui ya kutosha, yenye ubora na yatakayoweza kuvifanya vyombo vya habari viweze kuhimili ushindani pia” alisisitiza Matere...

SIMBA KUMCHUKUA SHEDRACK NSAJIGWA

Image
Siku chache baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa kuichezea klabu ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya mazungumzo na klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania wapo tayari kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars. Simba ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo. Mtoa taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano, na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika tutafanikiwa."

SAFARI WEZESHWA ARUSHA

Image
  Ofisa Biashara wa Manispaa ya Arusha, Niarira Magunda(kulia) akimkabidhi Mjasiliamali, Sofia Khalfan, Mashine ya kusaga wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa katika Viwanja vya Soweto Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.Kutoka Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiliamali, Veronica Mwamunyange,M          eneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda wa TBL, Kitio Wilderson. ******* Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)kupitia Bioa yake ya Safari Lager imekabidhi vitendea kazi mbalimbali kwa wajasiliamali 11 walifuzu kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa vyenye thamani ya shilingi milioni 50. Akizungumza katika sherehe ya makabidhiano ya vifaa hivyo jana jijini Arusha katika viwanja vya Soweto Meneja wa Safari Lager Bw.Oscar Shelukindo alisema kuwa shindano hilo la Wezeshwa na safari Lager nia yake kubwa nikuwapatia ruzuku wajasiriamali wadogo na wakati kuendeleza biashara zao. .Shelukind...
Image
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimpa pole Mbunge wa  Rombo, Joseph Selasini, wodini, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, leo. Selasini amehamishiwa Muhimbili kutoka KCMC, kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mkono alioumia katika ajali aliyopata hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita
Image
  Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuongoza shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chadema na Naibu Gavana wa benki kuu wa zamani, Bob Makani, leo. Wanaomkaribisha ni viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.   Rais Kikwete akiwa na viongozi wa Chadema, Mbowe, Dk. Slaa na Zitto Kabwe   Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, na Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.   Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimsalimia  Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta   Mwenyekiti wa IPP, Reginard Mengi akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi kwenye msiba huo   Dk. Slaa akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alipowasili kwenye msiba huo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar ...