SAFARI WEZESHWA ARUSHA
Ofisa
Biashara wa Manispaa ya Arusha, Niarira Magunda(kulia) akimkabidhi
Mjasiliamali, Sofia Khalfan, Mashine ya kusaga wakati wa kukabidhi
ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa katika Viwanja vya Soweto
Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.Kutoka Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya
Ujasiliamali, Veronica Mwamunyange,M eneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda wa TBL, Kitio Wilderson.
*******
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL)kupitia Bioa yake ya Safari Lager imekabidhi
vitendea kazi mbalimbali kwa wajasiliamali 11 walifuzu kupewa ruzuku za
Safari Wezeshwa vyenye thamani ya shilingi milioni 50.
Akizungumza
katika sherehe ya makabidhiano ya vifaa hivyo jana jijini Arusha katika
viwanja vya Soweto Meneja wa Safari Lager Bw.Oscar Shelukindo alisema
kuwa shindano hilo la Wezeshwa na safari Lager nia yake kubwa
nikuwapatia ruzuku wajasiriamali wadogo na wakati kuendeleza biashara
zao.
.Shelukindo
alisema jumla ya shilingi milioni 50 zimetumika katika kununulia vifaa
hivyo kwa ukanda wa kaskazini, ambapo mwaka 2011 ruzuku ilikuwa ni
milioni 200 kama vifaa vya vitendea kazi kwa wajasiriamali hao
walioshinda katika shindano hilo.
Alisema
kuwa zoezi hilo lilianzia mbeya na Arusha na wanatarajia wiki ijayo
kuwa Mwanza na mwisho kumalizia zoezi hilo Dar es Salaam.
Naye
Mgeni rasmi katika sherehe hizo,Niarire Magunda ambaye ni Afisa
Biashara Manispaa ya Arusha aliipongeza TBL kupitia Bia yake ya Safari
Lager kwa kuanzisha programu hiyo yenye nia ya kuwasaidia wajasiriamali
wadogo na wakati.
“Hakuna
mtu aliye maskini, kubwa nikuwezeshwa namna ya kupata fedha hivyo ni
vyema kama mtu akapata wazo la ujasiriamali ni bora akafanyia kazi wazo
lake ”alisema Magunda.
Hata
hivyo katika zoezi hilo wajasiriamali 11 kutoka Arusha,Moshi na Tanga
walikabidhiwa vifaa mbalimbali vya vitendea kazi, ambapo wajasiriamali
hao ni Bi.Ansilla Danny,Bi.Msuma,Bw.Roger Msangi,Bw.Simon
Kinabo,Bi.Sophia Khalfani,Bw.Yuda Mbando,Bi.Amina Lyimo,Bw.Adam
Akilinyingi,Bw.Joseph Mnemwa,Bi Rose Tesha na Bi.Victoria Tesha