SIMBA KUMCHUKUA SHEDRACK NSAJIGWA

Siku chache
baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa kuichezea klabu
ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya mazungumzo na
klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya
usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania wapo tayari
kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.
Simba
ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said
Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata
Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba
mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.
Mtoa
taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa
na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama
yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano,
na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika
tutafanikiwa."