KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimpa
pole Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, wodini, katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, leo. Selasini amehamishiwa Muhimbili
kutoka KCMC, kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mkono alioumia katika ajali
aliyopata hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es
Salaam, John Guninita
MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO
Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao . Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia. Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu. Njia za kukusaidia 1. ...