Posts

IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE, MUSEVENI,KAGAME,NA RAIS KABILA WAKUTANA JIJINI KAMPALA KATIKA MKUTANO WA MAZIWA MAKUU.

Image
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakifurahia  jambo wakati wa mkutano wa Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda.  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto),Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda(Watatu kulia) na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika mkutano wa viongozi wan chi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda jana jioni.Picha na Freddy Maro-IKULU

PINDA ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE ARUSHA

Image
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikagua mazao ya mbogamboga wakati alipotembelea maonesho ya wakulima  Nanenane kwenye uwanja vya Themi, Arusha Agust  8, 2012. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)  Mkuu Mizengo Pinda akifurahia mzinga wa nyuki aliozawadiwa na TASO katika maonesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Themi Arusha Agust 8,  2012.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kiolimo na Chakula na Ushirika, Adam Malima (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK BILAL AFUNGA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo  katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012 ...

MSAMA PROMOTION WACHARUKA

Image
Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani akifafanua jambo kwa Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tukio zima la kama kamata ya wezi wa kazi za wasanii iliofanyika mjini Dodoma. Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani mwenye fulana ya mistari akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) Cd za video na Audio Cd za Muziki wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye  kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma,mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaka na kuwakamata wezi  wa kazi za wasanii,ambapo jumla ya Cd na Computer zenye thamani ya shilingi milioni Sitini na saba zilikamatwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi mkoani humo.(PICHA ZOTE NA DIRA MEDIA)

SIMBA DAY YADORORA

Image
Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Nairobi City Stars katika mchezo wa kirafiki wa tamasha la Simba Day lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tamasha, hilo limeandaliwa na klabu ya Simba na hufanyika  kila mwaka Agosti 8 na kushirikisha timu marafiki wa klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo, hivi sasa mpira umekwisha na Simba imefungwa magoli 3-1 na timu  ya Nairobi City Stars kutoka nchini Kenya.  Benchi la ufundi la timu ya Nairobi  City Stars kutoka nchini Kenya kama linavyoonekana. Benchi la ufundi la timu ya Simba kushoto ni kocha wa timu hiyo Bw. Milovan Cirkovic Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo kiliongozwa na Juma Kaseja( GK) Kikosi cha timu ya Nairobi City Stars kutoka Kenya kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo. Mchezaji wa timu ya ...

MIFUGO

Image
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Meatu alipotembelea pori la akiba la Maswa.Nyuma yake ni mbunge wa jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu. Mkuu wa wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini akitoa taarifa yake ya maendeleo ya pori la akiba Maswa kwa naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aliyetembelea pori hilo. Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu Mh. Mpina akitoa salamu zake kwa wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa. Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa. Naibu Waziri wa Maliasli na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu (kushoto) akibadilishana mawazo na mbunge wa jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu Mh. Mpina muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa pori la akiba la Maswa. Baadhi ya viongozi waliofuatana na naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu kwenye boti kwenda kukagua mae...

MSAADA KWADELO

Image
  Mama Maria akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo .   Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho  kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.   Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.   Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama kijijini kwake   Omary Kariati diwani wa kata ya kwadelo,wilayani kondoa mkoa wa Dodoma akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni M...