Posts

USAHILI WA EPIC BONGO STAR SEARCH JIJINI DODOMA

Image
Majaji wakifanya majadilianokalbla ya kuanza kwa usaili huo uliofanyika mjini Dodoma jana kutoka kulia ni jaji Salama Jabir, Mkurugenzi wa Benchmark Production na Master J. Washiriki wa uasili huo wakiwa katika mstari wakisubiri wakisubiri taratibu zikamilike ili waanze kufanya uasaili Mawakala wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel wakiwapa huduma wateja wo kuhusu huduma ya kifedha ya Ezy Pesa katika ukumbi wa  Royal Village mjini Dodoma Mshiriki Fabian Peter Kikoko akitoa burudani wakati washiriki wakisubiri kuingia kwa majaji ili kuanza usaili.

MATUKIO MBALI MBALI KATIKA MSIBA WA WILLY EDWARD OGUNDE

Image
Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward ukuwasili Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam kuhifadhiwa, ukitokea Morogoro alikopatwa na mauti jana. Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (kulia) akimfariji mdogo wa marehemu Willy Edward, Ezekiel Ogunde Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa karibu na Mochuari Hospitali ya Muhimbili ulikohifadhiwa mwili wa marehemu Edward Waandishi wa habari wa gaz\eti la jambo leo wakiwa na huzuni wakisubiri mwili wa marehemu Edward. Kultoka kulia ni Asma Mokiwa, Grace Gulisha na Joyce Ngowi Wanahabari wakimfariji mdogo wa marehemu Willy Edward, Ezekel Ogunde Waandishi wa habari, Asha Kigundula wa Jambo Leo na Mwani Nyangasa wa Mtanzania wakilia kwa uchungu .

UTEUZI ZANZIBAR

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kwa vyombo vya habari   imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu. Rais amenya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu kumi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Walioteuliwa kupitia nafasi hizo na nyadhifa zao za sasa kwenye mabano ni Balozi Seif Ali Idd(Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) Omar Yussuf   Mzee(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo). Wengine ni    Zainab Omar( Waziri wa Ustawi wa Jamii,Maendeleo Vijana Wanawake na Watoto), Ali Mzee Ali, Sira Mwam...

wanahabari wahudhuria mafunzo ya sensa mkoani morogoro

Image
Esta Zelamula ambaye ni mhariri kutoka Channel 10 akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu uliofanyika jana mjini Morogoro. Zaidi ya shilingi bilioni 141 zitatumika katika zoezi hilo. Mussa Twangilo ambaye ni mhariri kutoka TBC Taifa akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo wa siku moja ulifanyika jana mjini Morogoro. Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akiwaonyesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi (hawapo pichani) kitabu cha ufafanuzi wa maswali ya sensa ya watu na makazi mwaka 2012. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uli...

TANZIA

Image
Bodi ya Wakurugenzi na wafanyakazi wa Jambo Concepts Ltd inayochapisha gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand wanapenda kuwajulisha Watanzania na wanahabari wote nchini kwamba Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro. Tunasikitika mno kuondokewa na mfanyakazi wetu ambaye alikuwa mchapakazi na mwenye ueledi mkubwa katika tasnia ya uandishi wa habari. Kwa wanaomfahamu Willy watakuwa mashahidi wa hilo tunalosema. Hadi sasa hatujapata taarifa rasmi za kidaktari kuhusu kifo chake, lakini taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu zinasema alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo. Mwili wa marehemu utawasili leo, Juni 17, 2012 na maandilizi ya mazishi yanaendelea.  WasifuWilly Edward Daniel Ogunde ambaye alikuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo alizaliwa Machi 7, 1974 katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara. Alisoma shule ya msingi Mapinduzi mwaka 1983 hadi 1989 kisha elimu ya Sekondari katika shule ya Serengeti mwaka ...

NBC YASHINDA

Image
Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Hussein Shabani (kulia) akigombea mpira  na Henry Justin wa timu ya Barclays katika mechi ya kirafiki  iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2. Wachezaji wa timu ya soka ya NBC wakishangilia baada ya kuibuka kidedea kwa kuinyuka timu ya Barclays kwa mabao 4-3 katika mchezo wa soka wa kirafiki jijini Dar es Salaam mwishoni leo. Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Ibrahim  Makoye (kulia) akimiliki mpira mbele ya Khatibu Shilumba wa timu ya Barclays katika mchezo wa kirafiki  uliofanyika katika Viwanja vya TCC Club, Chang’ombe, Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa penalti 4-3. Mkurugenzi wa Technolojia Habari wa Barclays, Dakshit Pandya (katikati) akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa nahodha wa timu ya soka ya Benki ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wao wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. K...

VODACOM YAFUNIKA COCO BEACH LEO

Image
Mmoja wa wakazi wa jijini Dares Salaam aliefika Coco-Beach kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la”WAJANJA”Linaloendeshwa na Vodacom Tanzania akipata huduma ya Vodacom Dstv,Tamasha hilo litafanyika   katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure. Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda akiongea na waandishi wa habari waliofika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la”WAJANJA”Coco Beach jijini Dares Salaam leo,Tamasha hilo linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,Tamasha hilo litafanyika   katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure. Umati wa wakazi wa Jiji la Dares Salaam waliojitokeza katika uz...