wanahabari wahudhuria mafunzo ya sensa mkoani morogoro
Esta
Zelamula ambaye ni mhariri kutoka Channel 10 akiuliza swali wakati wa
mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya
watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka
huu uliofanyika jana mjini Morogoro. Zaidi ya shilingi bilioni 141
zitatumika katika zoezi hilo.
Mussa
Twangilo ambaye ni mhariri kutoka TBC Taifa akiuliza swali wakati wa
mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya
watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka
huu. Mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo wa siku moja
ulifanyika jana mjini Morogoro.
Afisa
Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Said Amir akiwaonyesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi
(hawapo pichani) kitabu cha ufafanuzi wa maswali ya sensa ya watu na
makazi mwaka 2012. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ulioandaliwa na ofisi ya Taifa ya
Takwimu uliyofanyika mjini Morogoro.
Mtakwimu
Mohamed Kilonzo kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akiwaelekeza
wahariri na waandishi wa habari waandamizi jinsi ya kujaza dodoso refu
litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika
kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Wanahabari hao
walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka
2012 iliyofanyika jana mjini Morogoro.
Afisa
Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Said Amir akifurahia jambo wakati akiwaonyesha wahariri na waandishi wa
habari waandamizi (hawapo pichani) dodoso refu litakalojazwa wakati wa
sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia
tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Zaidi ya shilingi bilioni 141
zitatumika katika zoezi hilo.
Baadhi
ya wahariri na waandishi wa Habari waandamizi wakiangalia na kujaribu
kujaza dodoso refu litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi
inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka
huu. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu
na makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro ambapo mada
mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo.
Baadhi
ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi waliohudhuria mkutano
wa siku moja wa sensa ya watu na makazi uliofanyika jana mjini Morogoro
wakisikiliza mada ya nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha
sensa ya watu na makazi mwaka 2012 iliyotolewa na Afisa Uhamasishaji
sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir.
Zaidi ya shilingi bilioni 141 zitatumika katika zoezi hilo.Picha na Anna
Nkinda - Maelezo