UTEUZI ZANZIBAR

Rais
wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Marina Joel
Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa
ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya
Mzee kwa vyombo vya habari imesema
uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu.
Rais
amenya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba
ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu
kumi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Walioteuliwa
kupitia nafasi hizo na nyadhifa zao za sasa kwenye mabano ni Balozi Seif Ali
Idd(Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) Omar Yussuf
Mzee(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo).
Wengine
ni Zainab Omar( Waziri wa Ustawi wa
Jamii,Maendeleo Vijana Wanawake na Watoto), Ali Mzee Ali, Sira Mwamboya (Naibu
Waziri wa Afya) Juma Duni Haji (Waziri wa Afya), Fatma Abdulhabib
Ferej(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) Ramadhan Abdallah
Shabaan( Waziri wa Ardhi, Maji na
Maendeleo ya Makaazi) na Marina Joel Thomas.
Kikao
cha Baraza la Wawakilishi kinatarajiwa kuendelea kesho kwa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi kuanza kujadili bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
iliyowasilishwa Jumatano wiki hii.
Katika bajeti yake SMZ inatarajia kutumia
jumla ya TZS 648.9 bilioni katika mwaka wa fedha wa 2012/13, ikiwa ni ongezeko
la asilimia 38.2 kutoka shilingi 469.4
bilioni zinazotarajiwa kutumika hadi kufikia mwisho wa Juni mwaka huu.
Serikali pia inatarajia kuanza mwaka wa fedha
ikiwa na bakaa ya shilingi 5.9 bilioni. Katika hotuba yake Waziri nchi Ofisi ya
Rais anayeshughulikia Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee
alisema kwa kuzingatia uwezo wa sasa wa Serikali katika mapato yake kutokana na vyanzo vya ndani, yanatarajia
kufikia jumla ya shilingi 280.7 bilioni na hivyo kufanya jumla ya mapato
hayo kufikia shilingi 286.6 bilioni.