Posts

CLOUD'S MEDIA GROUP WATOA MSAADA

Image
Uongozi wa kampuni ya Clouds Media Group,Wasaniii wa muziki wa kizazi kipya na filamu,mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,walezi sambamba na watoto wa kituo hicho wakiwa katika picha pamoja. Baadhi ya vijana walioko kwenye mafunzo ya kujitolea kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo hicho cha matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.  Uongozi wa Clouds Media Group kwa kushirikiana na Baadhi ya wasanii wanaotumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakikabidhi sehemu ya misaada mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha The Village of Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma,kutoka kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Shetta,Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simalenga,mmoja wa walezi wa kituo hicho,Sister Maria Rosaria sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Benjamin Gembe wakiwa na watoto wa kituo hicho cha The Village of Hope baada ya kukabidhiwa msaada huo ambao walifurahia kuwa ki...

UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI TAIFA LEO

Image
Msanii wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu  ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.  Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Ne...

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)

Image
HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T) KWENYE UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWAUSALAMA BARABARANI KITAIFA MKOANI IRINGA TAREHE 17 SEPTEMBA, 2012 Mhe. Mgeni Rasmi Mhe. Eng. Gerson  Hosea Lwenge (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Ndugu Mbarak Abdulwakil, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Herbert Mrango, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Said Ally Mwema, Inspekta Jenerali wa Polisi Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani (T) Wageni Waalikwa Wanahabari Mabibi na Mabwana Asalaam Aleikum, Amani ya Mungu iwe juu yenu Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako Mhe. Mgeni rasmi kwa kukubali kwako  kuungana nasi katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho...

MAANDALIZI YA MKUTANO

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.   Na.MO BLOG -Arusha Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha nchini Tanzania kuanzia kesho hadi tarehe 14 mwezi huu.   Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine.  Mkutano huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na serikali yenyewe.   Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban dola za kimarekani 350,00...

MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA

Image
Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake. Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake. ************* MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA   KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA  Kanisa katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba. Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu. Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa. Akizungumza katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, As...

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo. Lengo kuu la ziara yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.  Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo. Hata hivyo baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja n...