Posts

MAGAZETI YETU KUANZIA 27 AUGUST

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

KOMBAINI COPA COCA-COLA YAENDA AFRIKA KUSINI

Image
Kombaini ya Copa Coca-Cola Tanzania (Dream Team) yenye wachezaji 16 inatarajia kuondoka kesho (Agosti 28 mwaka huu) asubuhi kwenda Afrika Kusini kwenye kambi itakayokuwa chini ya makocha wa Chelsea.   Makocha watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo watakaoongoza kambi maalumu ya kimataifa ya Copa Coca-Cola yenye wachezaji 140 kutoka nchini 15 itakayofanyika jijini Pretoria kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.   Robert Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo la makocha litakalowanoa vijana hao wenye umri chini ya miaka 17.   Wachezaji wanaounda Dream Team iliyotokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 24 hadi Julai 15 mwaka huu ni Abrahman Said Mohamed (Zanzibar), Ayubu Alfan (Dodoma), Baker Hamad (Tanga), Edward Joseph (Ruvuma), Hassan Kabunda (Temeke) na Jos...

Serengeti Fiesta 2012 yaanza kwa kishindo mjini Moshi

Image
Wasanii machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo limebamba ile mbaya.  Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo. Sehemu ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi. Mmoja wa wasanii w...