Posts

OMOTOLA KATIKA UMANJA WA JK

Image
Mwigizaji Omotola Jalade wa pili kushoto akikabidhiwa zawadi na za khanga, shanga na viatu Wema Sepetu wakati akiondoka kuelekea Nigeria jana usiku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole ambao waliratibu ziara ya msanii huyo. Mwingine wa msanii Snura.  Omotola akijaribu bangili za kimasai alizopewa kama zawadi 

Wageni watekwa wakiwa kambini Kenya

Image
  Polisi nchini Kenya wamesema kuwa wafanyikazi sita wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Ifo ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. kambi hiyo inatoa hifadhi wakimbizi nusu milioni Waliotekwa ni wafanyikazi wa shirika la Norwegian Refugee Council, ambalo linatoa huduma kwa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi kwenye kambi hiyo.   Msemaji wa Shirika hilo, amedhibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa katibu mkuu Elizabeth Rasmussen alikuwemo kwenye msafara uliovamiwa lakini amenusurika. Hata hivyo shirika hilo halijatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na watu waliotekwa. Mkuu wa wilaya ya Lagdera ambako kambi hiyo ipo Robert Kimanthi amesema waliotekwa ni raia wa Canada, Norway, Mfilipino, Mpakistani na Wakenya wawili. Wote ni wanaume. Kulingana na polisi watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walishambulia msafara wa magari katika kambi hiyo ambayo inatoa makaazi kwa zaidi ya wakimbizi nusu milioni kuto...
Image
Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).   Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.   Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.   ...

RATIBA YA KAGAME CUP

Image
Sat. 14 th July   1  APR vs WAU SALAAM          Uwanja wa Taifa            2pm                        2 YANGA vs ATLETICO           Uwanja wa Taifa            4pm   Sun. 15 th July   3 AZAM vs MAFUNZO             Chamazi                          4pm   Mon. 16 th July   4 VITA CLUB vs PORTS           Uwanja wa Taifa            2pm ...

Wahamiaji 42 wafa kwenye lori Tanzania

Image
Tanzania Wahamiaji haramu arobaini na wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori walimokuwa wakisafiria katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania. Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Pereira Silima, amesema kuwa watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya lori waliaga dunia kutokana ukosefu wa hewa safi. ''Taarifa tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC. wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi. Kulingana na bwana Silima wahamiaji hao walianza kufariki dunia wakiwa safarini. Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha dereva kuhusiana na hali yao hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa ya watu arobaini na moja ndani ya lori hilo. Kulingana na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani tukio hilo lilifanyika Jumatatu usiku. Na ba...

Ufadhili wa silaha waleta vita S Sudan

Image
Wanajeshi wa Sudan Kusini Silaha kutoka China, Ukraine na Sudan zinachangia machafuko Sudan Kusini. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International. Ripoti ya shirika hilo imesema raia wameendelea kuawa na kujeruhiwa kiholela kwenye makabiliano kati ya kundi moja la waasi na jeshi la Sudan Kusini. Amnesty International inasema silaha kutoka Sudan, mabomu ya kutegwa arthini kutoka China na Vifaru vilivyoagizwa Ukraini zimeendelea kutumiwa nchini humo. Hakuna upande ambao umejibu madai ya ripoti hii.   Vifaru vya Jeshi la Sudan Kusini vilitolewa kwa lililokua kundi la SPLA kati ya mwaka 2007 na 2009 kutoka Ukraine na kupitishiwa Kenya.Shirika hilo linaendelea kusema ,kampuni za Ujerumani na Uingereza ndizo zilihusika na usafirishwaji wa silaha hizo. Kutolewa kwa silaha hizo kulifanyika licha ya kuwepo mkataba wa amani wa mwaka 2005 pamoja na marufuku ya silaha iliyowekewa Sudan nzima.Ripoti ya Amnesty International ...

CHAMELEONE KUTUA BONGO

Image
Msanii wa Uganda, Jose Chameleone (pichani juu) leo amekamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa Taifa mpya, jijini Dar es salaam, siku ya sabasaba baada ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, kutia timu Entebe mapema leo. Pichani chini ni Chameleone akijigamba kufanya shoo na akisaini mkataba wa mwisho huku akishuhudiwa na meneja wake. Chameleone ametoa onyo kwa Diamond kuwa atamchakaza na Valuvalu!