Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao . Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia. Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu. Njia za kukusaidia 1. ...
Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012. Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana (21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu. Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu. Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni. Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vija...
HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T) KWENYE UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWAUSALAMA BARABARANI KITAIFA MKOANI IRINGA TAREHE 17 SEPTEMBA, 2012 Mhe. Mgeni Rasmi Mhe. Eng. Gerson Hosea Lwenge (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Ndugu Mbarak Abdulwakil, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Herbert Mrango, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Said Ally Mwema, Inspekta Jenerali wa Polisi Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani (T) Wageni Waalikwa Wanahabari Mabibi na Mabwana Asalaam Aleikum, Amani ya Mungu iwe juu yenu Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako Mhe. Mgeni rasmi kwa kukubali kwako kuungana nasi katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho...