TIGO YATOA MSAADA
Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa akiongea na waandishi wa
habari jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Holiday Inn wakati alipopokea
Hundi ya kiasi cha Shilingi milioni 26 kutoka kampuni ya Tigo kwa ajili ya kuchangia
Madawati katika Shule za Msingi 5 kutoka wilaya mbili Njombe na Makete zilizopo mkoani Iringa
ambapo alisema kuwa shule zitakazo faidika ni Maendeleo watapata madawati 135,
Umoja 196, Kumbila 200, Makonde 152 na Mbela 37. Aliongeza kuwa shule hizo
zimechaguliwa kulingana na kuwepo kwa
haja kubwa zaidi ya Madawati katika picha wa kwanza
kushoto ni Kaimu Meneja mkuu wa Tigo Bw,
Andrew Hadgson watatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya kupekea michango ya
kusaidia katika sekta ya Elimu Hassan Maajar Trust Zena Tenga wane kwenda kulia ni Mwenyekiti wa
kamati madawati Balozi Betha Somi wamwisho ni Dkt, Sinare Yusuf Sinare
Mwenyekiti wa kamati wa ukusanyaji Fedha taasisi ya Hassan Maajar Trust
Waziri
wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 26 kutoka
kwa Dkt, Sinare Yusuf Sinare Mwenyekiti wa kamati wa ukusanyaji Fedha
taasisi ya Hassan Maajar Trust
iliyotolewa na Kampuni ya Tigo ambapo fedha hizo zilipatikana katika
mfuko wa matembezi ya Hiyari ya Tigo
tuchange kwa Hassan Maajar Trust.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo jana.