KUTUMA PESA BUREEE
Kupata huduma ya Airtel money sasa piga *150*60# Bure
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa
kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure
Akiongea wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu
kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa
mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma na kuweza kuchagua
anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo,
kutoa pesa na mengine mengi
tumefanya hivi hii
ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na
kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa
kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye
muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja
vilevile
tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo
kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja
atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya
miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu
waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi
aliongeza” Mmbando
Airtel ni mtandao
ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye
mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini
kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za
kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma
za kibenki.