WAZIRI FENELLA AFUNGUA MASHINDANO YA UMISETA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara akishuhudia gwaride la maandamano ya
wanafunzi wa shule za sekondari wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya
shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani.
(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya shule
za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati
wa uzinduzi wa mashindano hayo,uzinduzi huo ulifanyika jana Mkoani Pwani.
(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akiongea na wachezaji wa Umoja wa Michezo wa shule
za Sekondari Tanzania (UMISETA) (hawapo pichani) wakati alipokwenda
kuzindua mashindano hayo Kibaha mkoani Pwani.Kushoto kwake ni Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Jumanne Sagini. (Picha na
Benjamin Sawe wa WHVUM)
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya michezo
mbalimbali ya shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakimsikiliza
kwa makini Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya shule za Sekondari
Tanzania (UMISETA). (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)