Skip to main content
WABUNGE KIBAO KUMSINDIKIZA SUGU
WAKATI
maandalizi ya shoo bab’kubwa ya muziki wa Hip Hop iliyopewa jina la
Usiku wa Sugu, yakiwa yameshakamilika, wabunge kibao, bila kujali
itikadi za vyama vyao wameahidi kujitokeza kumsindikiza mbunge mwenzao,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ atakayeongoza shoo hiyo ndani ya Ukumbi wa Dar
Live, Mbagala Zakhem.
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu kutokea
nchini Switzerland alikoenda kujifua sambamba na kufuatilia fursa za
maendeleo kwa wananchi wake, Sugu atakayekamua na Profesa Jay na Juma
Nature, aliwataja wabunge watakaomsindikiza Jumapili hii (Juni 3, 2012)
kuwa ni Ester Bulaya, Idd Azzan, Amos Makala ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zitto Kabwe, Freeman Mbowe,
John Mnyika na wengine wengi.
“Tumeamua kumsindikiza Sugu katika shoo
ya Dar Live bila kujali itikadi zetu kwa sababu anatuwakilisha wabunge
wote. Kizuri zaidi kilichotufurahisha ni kwamba mapato yatakayopatikana
ameahidi kuyatumia kutunisha mfuko wa elimu jimboni Mbeya.
“Tunaamini
wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa karo,
watalipiwa na shoo ya Usiku wa Sugu, kwa kweli ametufurahisha sana,
lazima tumuunge mkono Jumapili hii,” alisema mbunge mmoja wa chama
tawala kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini