VIONGOZI WA BENDI ZA DANSI WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Kiongozi wa Bendi ya Muziki wa dansi ya Extra Bongo, Ally Choki (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu mkutano utakao husisha bendi mbalimbali na wadau wa muziki huo
wenye lengo la kuinua wanamuziki chipukizi kupitia vyombo vya habari na
masuala mengine. Kushoto ni mmoja wa kiongozi wa bendi ya Njenje, John
Kitime na Meneja wa bendi ya Mapacha watatu, Khalid Chokoraa.