UMOJA WA VYAMA VYA SIASA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI
Katibu Mkuu wa Chama cha siasa TADEA Juma Ali Khatibu akizungumza na
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali hawapo pichani kwa niaba ya
Umoja wa Vyama vya TADEA,SAU,NLD na AFP kuhusiana na kuimarisha Amani na
Utulivu Zanzibar na Kulaani matukio ya uvunjifu wa Amani yaliotokezea
hivi karibuni huko Zanzibar.
Na
Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Vyama
vitano vya siasa vimesema mafanikio ya kukua kwa uchumi wa Zanzibar ni matokeo ya kushamiri kwa
amani,utulivu na mshikamano wa wananchi.
Wakizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Mjini Zanzibar, Viongozi wa Vyama vya TADEA,AFP, NLD, SAU, kwa pamoja
vimeridhishwa na ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa pato la wananchi.
“Mafanikio
ya kukua kwa uchumi wetu yanaendelea kutupa funzo juu ya umuhimu wa kuilinda
amani, utulivu na mshikamano wetu ambao umetujengea sifa kubwa” Alisema Katibu
Mkuu wa TADEA, Juma Ali Khatib.
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi wenzake katika mkutano huo, Katibu Mkuu huyo wa TADEA
alisema taarifa za uchumi zinaonesha kuwa Zanzibar
imepata mafabnikio katika kukuza uchumi.
“Kwa
mujibu wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013, pato la mtu mmoja limeongezeka
kutoka wastani wa shilingi 782,000 mwaka 2010 na kufikia shilingi 960,000 mwaka
huu” Alisema Kiongozi huyo.
Alisema
hayo ni mafanikio makubwa. “Kwa wenzetu hawa wa Chama Tawala-CCM tayari
wameshavuka lengo lao la miaka mitano katika muda wa miaka miwili tu…wao
walilenga pato la mwananchi lifikie wastani wa shilingi 884,000 ifikapo mwaka
2015” Aliongeza Juma Ali Khatib.
Kutokakana
na mafanikio hayo, vyama hivyo vimetoa shutuma kwamba kuna mkono wa kisiasa
unaolenga kuvuruga mafanikio yaliyokwisha patikana na ndio maana kumekuwa na
matukio vurugu katika siku za hivi karibuni.
“Hapa
ndipo inapokuja hofu kwamba kuna mkono wa siasa kuvuruga mafanikio haya hasa
kwa vile hayo ni matunfa yanayotokana na hali ya amani,utulivu na mshikamano wa
Wazanzibari ambapo wananchi waliweza kuendelea na shughjuli zao za uzalishaji
na biashara bila usumbufu,wageni waliendelea kufurika nchini na wawekezaji
wameendelea kuwekeza” Alisema Katibu Mkuu wa TADEA.
Vyama
hivyo, pia vimewakumbusha wananchi ulazima wa kuilinda amani iliyopo na
kutokubali kutumiwa na watu wasioitakia mema Zanzibar.
Katika
hatua nyengine katika tamko la vyama hivyo
vimeituhumu Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam kwenda kinyume na
masharti ya uanzishwaji wake na kuiomba Serikali kuangalia usajili wa Jumuiya hiyo.
Aidha,
imewasihi Mashekh na Maulamaa wote wasitumi dini kama
ngao ya kuwapotosha wananchi na kusababisha vurugu ndani ya nchi. “Tunawaomba
wananchi walioanza harakati za kutaka kuigawa nchi kwa misingi ya uzawa
kuachana na kasumba hizo kwani hazina
hatma njema miongoni mwa Wazanzibari” Limesisitiza tamko la vyama hivyo.