TUKIO MAALUMU

MNAMO TAREHE 06/06/2012 MUDA WA SAA 11:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA OLKEIJULONGISHU KATA YA OLKEJULONGISHU WILAYANI LONGIDO, MWANAMKE AITWAYE NEISISIRI D/O PARAMETI MOKOROO (25) MFUGAJI NA NI MKAZI WA KIJIJI CHA OLKEIJULONGISHU ALIFARIKI DUNIA BAADA YA MUME WAKE AITWAYE KAPAITO S/O NAANJARATI (UMRI BADO HAUJAJULIKANA) MFUGAJI , KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE.
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KWAMBA, TUKIO HILO LILITOKEA BAADA YA WATU HAO KWENDA SHAMBANI KUKATA NYASI NA WALIPOKUWA HUKO, NDIPO MTUHUMIWA AMBAYE NI MUME WA MAREHEMU KUMTUHUMU MKEWE KWAMBA, UJAUZITO ALIONAO SI WA KWAKE BALI AMEPEWA NA MWANAUME MWINGINE HALI ILIYOSABABISHA AANZE KUMPIGA KWA FIMBO NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO.
BAADA YA TUKIO HILO MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA HAJULIKANI ALIPO NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO LINAENDELEA KUMTAFUTA NA PINDI ATAKAPOPATIKANA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZINAZOMKABILI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA LONGIDO.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)