TTB WAFAGILIWA KWA KAZI NZURI
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarish (Kushoto)
akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii
Tanzania –TTB alipokuwa akifungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika
katika ukumbi wa chuo cha Utalii jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki, na kulia ni Katibu wa
Baraza hilo Bw Elirehema Maturo.
************
Na: Geofrey Tengeneza
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) imepongezwa kwa kazi nzuri inayofanya katika
utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na jukumu kubwa la
kuitangaza Tanzania kama eneo bora lenye vivutio vingi vya kitalii
duniani pamoja na ushindani mkubwa kutoka nchi nyingine na hivyo kufanya
idadi ya watalii wanotembelea nchi yetu kuendelea kuongezeka mwaka
hadi mwaka sambamba na kuongezeka kwa pato la Taifa litokanalo na sekta
ya utalii.
Akifungua
kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii hivi karibuni
katika ukumbi wa Mikutano wa chuo cha Utalii jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarish
amesema Bodi ya Utalii imeendelea kutekeleza vema majukumu yake na
kwamba wafanyakazi wa taasisi wana kila sababu ya kujivunia mafanikio
haya kwa kuwa kila mmoja kwa nafasi yake amechangia katika mafanikio
hayo.
Amewataka
wafanyakazi kuendelea kuwa wabunifu zaidi kwa kuibua mawazo mapya
yatakayosaidia kuboresha utendaji wa Bodi siku hadi siku na kujipima
kwa matokeo ya kazi na mipango wanayojiwekea. “Nawaomba sambamba na
kuwa na mipango ya kazi mfanye kazi kwa matokeo na kuwa wabunifu kadri
iwezekanavyo kwa kila mfanyakazi kujitahidi kuwa na mawazo mapya ambayo
yatasaidia shirika kuboresha utekelezji wa majukumu majukumu yake”
alisema Bibi Maimuna.
Akizungumzia
mikutano ya Baraza la Wafanyakazi sehemu za kazi Katibu Mkuu huyo
amesema jambo muhimu sana katika kutatua baadhi ya matatizo
yanayoikabili taasisi husika kwa kuwa mikutano hiyo ndicho chombo cha
juu kabisa ambacho wafanyakazi kupitia wawakilishi na viongozi wao wa
vyama vya wafanyakazi na Menejimenti wanapata fursa ya kukaa pamoja na
kujadili masuala mbalimbali yanayohusu taasisi na wafanyakazi kwa
ujumla.
Amesema
kwa kufanya hivyo ni kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali
linalolenga katika kuendeleza na kudumisha utawala bora jambo ambalo
linadumisha umoja na mshikamano baina ya wafanyakazi.
Baraza
hili jipya la wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na mambo
mengine kadhaa katika kikao chake hicho cha siku mbili lilipokea na
kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya Bodi katika kipindi cha
mwaka 2012/2013, na taarifa ya utekelezaji wa mipango na kazi mbali
mbali za Bodi katika kipindi cha Julai 2011 hadi Machi 2012.
Utalii
nii Sekta ya pili nchini kwa kuchangia katika pato la Taifa ambapo
inachangia kiasi cha asilimia 17.2 baada sekta ya Madini ambayo ndiyo
inaongoza. Aidha kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 idadi ya watalii
waliotembelea Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani iliongezeka
kutoka watalii 782,699 mwaka 2010 hadi watalii 867,994.
Nayo
mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Kimarekani
1,254.50 mwaka 2010 hadi ufikia dola za kimarekani 1,348,30