TEMEKE NA MBEYA NI MABINGWA
Nahodha
wa timu ya wasichana ya mkoa wa Mbeya Mariam Ndauka, akinyanyua juu
kombe baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa
wanawake baada ya kuifunga Arusha 1-0 kwenye fainali za Airtel Rising
Stars zilizofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam.
Time
ya Temeke ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka kuwa washindi wa
michuano ya Airtel Rising Stars kwa kutwaa ushindi wa mabao 3-1 thidi ya
timu ya Mbeya.
Wachezaji
nyota 6 wa michuano ya Airtel Rising stars wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kuchaguliwa jana katika michuano ya Finali
iliyofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.
Nahodha
wa timu ya wavulana ya Temeke Khalid Salum, akipokea kikombe kutoka
kwa Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamanduni na Michez,o Juliana Matagi Yasoda. Temeke iliibuka mshindi
wa michuano hiyo kwa wanaume baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali
iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume Jumapili 17 jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
bora wa michuano ya Airtel Rising Stars, Abdul Seleman wa timu ya
mkoa wa Temeke, akipokea kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF,
Sunday Kayuni. Michuano hiyo ilimalizika juzi kwenye Uwanja wa Karume
kwa Temeke kuibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Mbeya
magoli 3-1.
********
Temeke, Mbeya mabingwa michuano ya ARS.
Fainali
za taifa michuano ya Airtel Rising Stars iliyokuwa ikihusisha timu za
mpira wa miguu kwa timu za wavulana na wasichana, zilifikia tamati
Jumapili 17 kwenye Uwanja wa Karume huku timu za wavulana Temeke na
Mbeya wasichana zikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.
Michuano
hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 pia imetoa wachezaji sita
bora ambao watahudhuria kliniki ya soka ya Kimataifa itakayokuwa chini
ya walimu kutoka Klabu ya Manchester United ambayo itafanyika Nairobi.
Wachezaji hao ni – Jackline Gibson na Irene Bahisi kutoka Arusha,
Madeline Sylvester (Ilala), Abdul Seleman, Denis Richard na Paul Balama
(Temeke).
Jumla
ya timu za shule za sekondari 24 kutoka mikoa sita zilishiriki
michuano ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu huku wachezaji bora
wakichanguliwa kuunda timu kombaini za mikoa kwa ajili ya fainali za
taifa. Mikoa iliyoshiriki ni Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Kinondoni na
Temeke.
Shule
hizo zilichanguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya
taifa ya shule za sekondari (UMISSETA) mwaka jana. Uzinduzi rasmi wa
ARS 2012 ulifanyika Mei, kwenye Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es
Salaam na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya
Uingereza, Quinton Fortune.
Fainali
za ARS za wiki moja pia zimetumika kuchangua timu ambayo itawakilisha
Tanzania kwenye michuano ya ‘inter-continental’ ambayo itashirikisha
nchi 17 ambao Airtel inafanya biashara. Michuano hii itafanyika Nairobi
mwezi wa Agosti.
Timu
ya wavulana ya Temeke imepata nafasi ya kuwa bingwa wa Airtel Rising
Stars 2012 baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali kali y a kusisimua
huku wasichana wa Mbeya wakiibuka bingwa baada ya kuwafunga wenzao
Arusha 3-1. Timu hizo mbili bingwa zilijinyakulia vitabu vya thamani ya
Tshs1m, medali ya dhahabu na vyeti vya kushiriki.
Michuano
wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa
kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na
wasichana wenye miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda wa
kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao
watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel
Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza ya
Manchester United ya kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Huu ni mwaka
wa pili kwa Airtel kudhamini michuano hii. Mwaka jana, Klabu ya
Manchester United ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki
ya soka ya Kimataifa ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania, Afrika
Kusini na Gabon.