TBL YATOA MILIONI 200
Akikabidhi vitendea kaz i hivyo kwa wafanyabiashara wa kanda ya
kaskazini katika tamasha lililofanyika mjini hapa meneja wa bia ya
Safari larger Bw. Oscar Shelukindo alisema kuwa kampuni hiyo imejiwekea
mpango wa kuhakikisha kuwa wanawasidia wajasiriamali Tanzania nzima ili
waweze kujikwamua katika hali ngumu ya kiumskini.
Alisema kuwa vifaa hivyo walivyovitoa kwa wafanyabiashara hao ni
vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kutumika katika biashara zao mbali
mbali wanazoziendesha kwa kuwa wako watu wana malengo na maono mazuri ya
baishara lakini wanashindwa kufikia malengo kwa ajili ya kukosa
vitendea kazi.
“Sisi tumeona tuwe na mpango endelevu wa kuwasaidia hawa
wafanyabiashara vitendea kazi mfano yuko huyu mfugaji wa kuku tumempatia
mashine,mwingine friza ambapo kila mmoja anategemea biashara anayofanya
alimaradi tu wamekidhi vigezo vyetu lazima tumapatie vitendea kazi
“alisema Shelukindo
Aliongeza kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ambapo ametaja kanda
ambazo zinahusika na kupatiwa vitendea kazi kuwa ni pamoja na kanda ya
kusini ,Mwanza, Dares saalam pamoja na kanda ya kaskazini ambapo
aliwataka wafanyabiashara kujitokeza mwaka huu kujaza fomu kwa kuwa
endapo watakidhi vigezo vinavyohitajika nao wataweza kunufaika na
vitendea kazi vya kuendeshea biashara zao.
Awali mgeni rasmi katika tamasha hilo afisa biashara manispaa ya
arusha bw Niarira Elivelema alisema kuwa swala hilo lililofanywa na
Safari Larger ni mfano wa kuigwa na taasisi nyinginezo kwa kuwa
wameonyesha ushirikiano wao na jamii inayowazunguka .
Aliongeza kuwa endapo wafanyabiashara wadogo watapewa kipaumbele
kama walivyofanya tbl ni wazi kuwa hata taifa nalo litaweza kuongeza
kipato kutokana na ushuru ambao utakuwa unalipwa kutoka kwa
wafanyabiashara hao.