
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili mjini Abdijan nchini Ivory coast tarehe 31 May na pia kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa la Tanzania Kim Poulsen amesema mechi hiyo itakuwa ngumu kwao.Mechi hiyo ya mchujo wa kombe la Dunia itachezwa tarehe 2 June kwenye uwanja wa Felix Houphouet- Boigny saa kumi 11 kamili jioni ambapo kwa saa za Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.
Kikosi cha Taifa stars kinaongozwa na nahodha wake kipa Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris wengine ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi,Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondan, Waziri Salum,Shomari kapombe na Juma Nyoso.