SHEREHE ZA USHINDI WA CHELSEA UEFA
Kufuatia
mafanikio makubwa ya timu ya Chelsea kwa kutwaa kombe la Ligi ya
Mabingwa Ulaya, mashabiki wa Tanzania wa timu hiyo wameandaa sherehe
kubwa ya kusheherekea ubingwa huo iliyopangwa kufanyika kabla ya mwisho
wa mwezi huu.
Mashabiki
hao kupitia kamati yao maalum walifanya kikao jana kwenye hotel ya
Wanyama, Sinza Mori na kukutwa na blogu yetu. Kamati hiyo imeundwa na
wadau mbali mbali chini ya mwenyekiti, Katibu Mkuu wa zamani wa
Shirikisho la kandanda nchini, TFF, Fredrick Mwakalebela, Afisa Habari
wa zamani wa TFF, Florian Kaijage na mpenzi mkubwa wa michezo wa timu
hiyo, Rodrick Mwambene.
Wengine
wanaunda kamati hiyo ni Mmiliki wa kituo cha redio cha Times, Lehure
Nyaulawa, Mtangazaji wa Times FM, Clifford Ndimbo, Deogratius Rweyunga,
Peter Ngassa na wengine mbali mbali.
Wadau
hao walisema kuwa wana mipango mikubwa ya kuendeleza umoja wao na
Jumatatu watafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mipango
hiyo.
Walisema kuwa lazima wafanye sherehe ya ‘kufa mtu’ na wanataka kumwalika mmoja wa wachezaji wa timu hiyo kuhudhuria sherehe hiyo ya kwanza nay a aina yake hapa nchini.