PONGEZI KUTOKA KWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR
Makamo
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Ofisi ya Tume ya
Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) na Tume za Nguvu za Atomic (TAEC) kwa
uwamuzi wake wa busara kwa kuamua kufungua ofisi zao hapa Zanzibar
Pongezi
hizo alizitoa jana huko Tunguu wakati alipokuwa akizindua Ofisi hizo
alisema kuwa ni faraja kubwa kwa watu wa Zanzibar kupata huduma za Tume
ya Sayansi na Teknologia pamoja na Nguvu za Atomic hapa hapa Zanzibar .
Alieleza
kuwa tume hizo ambazo zimefungua ofisi zake hapa Zanzibar itasaidia
kuwapatia elimu mbali mbali wananchi wa Zanzibar wakiwemo wajasiri amali
ambao tayari wameweza kupata elimu ambayo imewafanya kuweza kuuuza
bidhaa zilizokamilika.
Aidha
akifafanua alisema kuwa bidhaa hizi ambazo zinatengenezwa na wajasili
amali zinawafanya waweze kupata manufaa ambayo huongeza harakati ya
maendeleo kiuchumi pamoja na kupunguza umasikini nchini.
Balozi
huyo alieleza kuwa tume hizi zitasaidia kutoa mchango mkubwa kwa
wananchi ikiwemo kuwapa elimu ya tafiti mbali mbali ikiwemo kilimo
kuweza kupata mbegu bora , utafiti wa afya ikiwemo maradhi ya saratani
,pamoja na athari ambazo zinapatikana kutokana na mionzi ambayo
inaitumiwa na wananchi katika shughuli zetu za kila siku ili kuweza
kujua athari hizo na kuweza kuziepuka .
Alifahamisha
kuwa shughuli za utafiti zina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya
nchi na umuhimu wake unaeleweka ambao ni mkombozi wa kuondoa dimbwi
la umasikini nchini .
Akifafanua
kuwa tume hizo zinategemea kuwashajihisha wasomi mbali mbali kufanya
utafiti katika nyanja tofauti kwa manufaa ya nchi.
Nae waziri wa
Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Makame Mbarawa Mnyaa alisema kuwa
Tume hizo zitaweka mashirikiano katika masuala ya ICTili kuikuza zaidi
chuo kikuu cha Suza ili kuweza kutoa elimu hiyo kwa ufanisi zaidi.
Aidha
alieleza kuwa Tume hizo tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya
kukifanyia matengenezo chuo cha kizimbani pamoja na kufanyia tafiti
mbalimbali.