PATA UFUMBUZI ZAIDI

JE WAJUA?
  • Poland ni mwenyeji mshiriki wa michuano hii ya Euro, wakishirikiana na Ukraine - hii ikiwa mara ya kwanza kwao kuandaa michuano hiyo mikubwa.
  • Tai Mweupe ilifuzu kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Ulaya mwaka 2008, lakini ikashika mkia kwenye kundi lake, kwa kuambulia pointi moja.
  • Poland imekutana na Ugiriki mara 15 na imewanyanyasa wapinzani wao hao wa Ulaya, ikiwafunga mechi 10, kutoka sare mbili na kufungwa tatu.
  • Vijana wa Smuda wameweka rekodi ya taifa ya kushinda mechi tano mfululizo, wakicheza dakika 461 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa, tangu wafungwe na 2-1 na Hungary, Novemba 15, 2011.
  • Ugiriki ilifuzu Euro 2012 kwa kuongoza Kundi F, ikimaliza na pointi 24 na haikufungwa hata mechi moja, ikifuatiwa na Croatia na Israel.
  • Kuna wachezaji watatu waliokujwamo kwenye kikosi cha ubingwa cha Euro 2004-katika fainali hizi za Poland na Ukraine: Giorgos Karagounis, Kostas Katsouranis (pichani kulia) na Kostas Chalkias.
  • Ugiriki bado haijaweza kuepuka vipigo vya Poland, na katika mechi nane wamefungwa zote, wakifunga mabao manne tu, wakati wao wamefungwa 22.
  • Karagounis ameichezea mechi 117 Ugiriki, anazidiwa tatu tu na Theodoros Zagorakis, ambaye anashikilia rekodi ya taifa.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)