NMB YAIPA WIZARA SH. BILIONI 7.9 KAMA GAWIO KWA SERIKALI

Mtendaji Mkuu wa Benki (Chief Executive Officer ) ya NMB Mark Wiessing (katikati) akimkabidhi  Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(wa pili kushoto) mfano wa  hundi ya shilingi bilioni saba nukta tisa(7.9 ) leo mjini Dar es salaam ikiwa ni gawio kwa Serikali ya Tanzania kutokana na faida iliyopata.  Wengini ni Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene (kushoto)  ,Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum (kulia) na Meneja Mwanandamizi anayeshughulikia masuala ya Serikali wa NMB Domina Feruzi.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha jana mjini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(wa nne kutoka kushoto) akiwa na Manaibu wake  Janet Mbene (wa tatu kutoka kushoto)  ,Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum (wan ne kutoka kulia) wakiimba maalum wa wafanyakazi wakati mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofunguliwa leo mjini Dar es salaam na Waziri huyo.
Mtendaji Mkuu wa Benki (Chief Executive Officer ) ya NMB Mark Wiessing (wa pili kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(wa pili kulia)jana mjini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya Benki hiyo  kukabidhi hundi ya shilingi bilioni saba nukta tisa(7.9 ) ikiwa ni gawio kwa Serikali ya Tanzania kutokana na faida iliyopata. Wengini ni Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene (kulia0 na Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum (kushoto).

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)