NEW TRACK
Kwa miaka nenda rudi sasa,Hamis Mwinjuma ambaye wengi wetu tunamuita MwanaFA au Binamu, amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba muziki wa kizazi kipya unabakia kuwa chaguo la wengi hivi leo.Anafanya hivyo sio kwa maneno bali kwa vitendo. Kila mara anajaribu kutunga kitu ambacho kitamfanya msikilizaji aburudike lakini wimbo unafikia mwisho,msikilizaji apate ujumbe na wasaa wa kutafakari.Ndio aina yake ya muziki ambayo imemfanya aendelee kukubalika hata baada ya miaka yote hii katika fani. Siku hizi mwenyewe ana msemo #KeepingTheGoodMusicAlive.
Ujumbe, burudani na fikra ndicho kilinijia baada ya kusikiliza wimbo ambao nawe msomaji utapata fursa ya kuusikiliza hivi punde. Ni wazi kwamba sisi sote,na ujanja ujanja wetu, tu watupu bila Mwenyezi Mungu ambaye ndiye muwezeshaji na kiongozi wa yote. Katika wimbo huu ambao MwanaFA amemshirikisha Dully Sykes(ambaye pia ni Producer wa wimbo huu) na swahiba wake Ambwene Yesaya(AY),huo ndio ujumbe na ombi. Kiitikio chake cha mwisho ni Ameen. Hilo ndilo jina la wimbo. Usikilize hapa chini kisha usome mahojiano yangu mafupi na MwanaFA juu ya wimbo huu na mengine machache juu ya muziki na kile ambacho mashabiki wa muziki watarajie kutoka kwake;
BC: MwanaFA,karibu sana…karibu tena!Mambo yanakwendaje?Ameen au sio?
MwanaFA: Asante bingwa,nipo…tunaendelea tu kujaribu kufanya tunachofanya kinavyostahili kufanywa…Mungu anatuongoza..
BC: Kuna kitu kama hasira hivi(sio hasira mbaya;hasira ya maendeleo) miongoni mwenu nyie ambao tunaweza kuwaita “wakongwe”. Mnashirikiana(hapa kuna wewe,Dully Sykes na AY) na kufyatua vitu “hatari”.Kuna ujumbe wowote ambao mnajaribu(kwa njia moja ama nyingine) kuupeleka kwa vijana wanaochipukia au wanaotaka kufikia pale mlipo?
MwanaFA: Ni kweli,pengine ujumbe haupo wazi kwa wanaotaka mpaka wasikie unataka kusema nini kwa kutamka.Lakini kimatendo tunachokisema ni kile kile,STAY HUNGRY KIDS..sio wasipate wanachostahili kukipata,laa hasha,ila waendelee kuwa na ‘hasira’ za kufanikiwa kama hawajatoka..
BC: Katika wimbo huu,Mwenyezi Mungu amewekwa mbele.Matumaini yote ni kwa Muumba.Akushike mkono akuongezee.Mabadiliko yoyote ya kiimani au matendo nk?
MwanaFA: Nionavyo,namna rahisi ya kupotea kwenye chochote unachokifanya,ni kuridhika na kujiona ‘umemaliza’..tunayo mifano mingi halisi..
Mungu amewekwa mbele kwenye “Ameen”,sio mabadiliko ya kiimani,ila ni kuona haja ya kuwakumbusha walimwengu kuwa Kila La Heri na Shari Duniani ni la Mwenyezi Mungu.Haijalishi unaomba nini na unawaombea nini wa upande wako na maadui zako vile vile.Mtoaji ni huyo huyo mmoja..hivyo wakumbuke kumtanguliza.Wewe na mimi tunafahamiana vyema,msimamo bado upo vilevile.Nakosea hapa na pale lakini simsahau Mungu,na bado naswali swala 5..
BC: Tunaposikia single kali kali kama hizi,huwa kuna hisia kwamba pengine kuna album ipo njiani. Lakini siku hizi,sio lazima sana kwani naambiwa shows zinalipa kuliko albums.Kwa upande wako imekaaje.Ameen ni teaser ya album au?
MwanaFA: Not exactly…najaribu kufanyia majaribio kamfumo kamoja ka biashara,so sisemi nafanya album kwa sasa.Nitakapokuwa tayari nitasema zaidi..kwa sasa tuseme tunakusanya nyimbo..
BC: Mtaani kuna maneno,kuna kitu kama re-union ya baadhi ya members wa East Coast.Kuna picha zimeonekana mkiwa studio na mambo kama hayo na mtu mzima Crazy GK na AY.Can you set the record straight? What is going on?
MwanaFA: East Coast Team, hili naomba niliruke.Kama kawaida ya tangu enzi,kama kuna lolote linalohusu ECT ni GK anayekuwa na jukumu la kuongea.So naomba nisimruke,atafunguka,very soon.Subira kidogo tafadhali..
BC: Kwa kuusikiliza,wimbo huu umejaa na umesheheni kwa maana ya beats, vionjo,mixing nk. Ni nani anahusika nyuma ya hili pazia?
MwanaFA: Huu wimbo umetengenezwa na Dully Sykes mwenyewe,kwenye studio yake aliyoibadili jina toka Dhahabu Records na sasa inaitwa Studio 4.12(December 4th)..
BC: Good job Bro.Keep the Good Music Alive.Pamoja
MwanaFA: Ahsante sana..wafikishie watu wetu wazidi kusikiliza na kutuunga mkono na we will keep the good music alive..Ameen..
Bless..