MWENDESHA MASHITAKA MPYA WA ICC
Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague hii leo.
Mojawapo wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gadaffi, ambaye ameshtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu na wakati huohuo kuongoza mashtaka yanayomkabili aliyekuwa kiongozi wa Ivory Coast, Laurant Gbagbo.
Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi wake aliyeondoka, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja.
Kesi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, ilisikizwa na mahakama mahakama ya Umoja wa mataifa inayosikiliza kesi za waliohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Sierra Leone.
Bi Bensouda amekuwa akihudumu kama naibu wa Luis Moreno-Ocampo anayemaliza kazi yake katika mahakama ya ICC.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa licha ya kwamba Bi Bensouda sio mgeni kwa mambo ya Hague, uteuzi wake unakuja wakati mfumo wa sheria ya kimataifa unahojiwa sana.
Pia anachukua jukumu hilo wakati kuna mtafaruku katika mahakama hiyo huku maafisa wanne wa mahakama hiyo wakiwa wanazuiliwa nchini Libya.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa Bi Bensouda anasifika kwa kuwa mtulivu kitu ambacho huenda kimemsaidia katika kazi yake.
Ikizingatiwa kuwa washukiwa wengi ambao sezi zao ziko katika mahakama ya ICC ni waafrika na hili limekosolewa huku ofisi ya mwendesha mkuu wa mashtaka ikisemekana kuwalenga zaidi waafrika.
Inatarajiwa kuwa kwa sababu Bi Bensouda mwenyewe ni Mwafrika tena wakili, huenda akasaidiwa na hili kunyamazisha wakosoaji wake, kulinagana na wadadisi.
Mwezi Machi mbabe wa kivita kutoka DRC, Thomas Lubanga alipokea hukumu ya kwanza ya kesi yake ikiwa hukumu ya kwanza kuwahi kutolewa na mahakama hiyo tangu kuundwa kwake miaka kumi iliuopita.
Kikosi cha viongozi wa mashtaka wanataka Lubanga apokee miaka 30 jela kwa makosa ya kutumia watoto kama wanajeshi wakati wa vita mashariki mwa nchi yo kati ya mwaka 2002 na 2003.