MTOTO WA MBUNGE WA TEMEKE(CCM) SITTI MTEMVU AMSAIDIA SH. 500,000 MSICHANA HAPPINESS KAAYA MLEMAVU ANAYEISHI NDANI KWA MIAKA 22
Mamake Sitti, Mariam Mtemvu, ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu ampa pole Happiness.
Sitti ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, akimbusu
Happiness baada ya kutoa msaada huo. Sitti pia ni mmoja wa wakurugenzi
wa Mtemvu Foundation
MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas cha Marekani, Sitti Mtemvu
(kushoto), akitoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya
(22), aliyezaliwa akiwa mlemavu, katika hafla iliyofanyika Machimbo,
Temeke, Dar es Salaam juzi.
Sitti akitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu,
Nassoro Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya
kununulia vipuri vya kutengenezea baiskeli yake.
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Happiness na mamake Khadija Msuya akielezea jinsi wanavyomsaidia msichana huyo mlemavu
---
Na Richard Mwaikenda
MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas, Marekani, Sitti Mtemvu, ametoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya (22), aliyezaliwa akiwa mlemavu.
Msaada huo alikabidhi kwa mama mzazi wa Happiness, Khadija Msuya katika hafla iliyofanyika kwenye chumba wanachoishi eneo la Machimbo, Temeke, Dar es Salaam juzi.
Siti ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mtemvu Foundation, alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na taarifa za msichana huyo alizozisoma kwenye mafaili ya mfuko huo, zilizopo Temeke, Dar es Salaam.
"Taarifa za msichana huyu, zilinigusa mno kuliko wengine, kiasi cha kuamua kuanza kutoa msaada kwa Happiness aliyezaliwa akiwa mlemavu na analelewa mamake kwa shida,"alisema Siti.
Siti ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, alisema kuwa fedha alizizitoa ni sehemu ya mapato yanayotokana na bajaji zake tatu zinazofanya biashara ya kubeba abiria jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Bajaji hizo alizinunua kutoka na na fedha alizolipwa baada ya kushiriki kwenye filamu moja nchini Marekani anakosoma.
"Sitoishia kutoa msaada kwa msichana huyo, bali nina imani Mungu akinijalia nitaendelea kutoa msaada kwa yatima na watu wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu"alisema Siti.
Mama mzazi wa Happiness, Khadija, alishukuru kupata msaada huo kutoka kwa Sitti, ambao alidai utamsaidia sana kupunguza baadhi ya matatizo yanayomkabili.
Alisema kuwa mtoto huyo ambaye alimzaa akiwa na ulemavu, hana uwezo wa kutembea ambapo hata kula chakula ni vigumu inabidi alishwe na kumsaidia wakati wa kujisaidia.
Alidai kuwa Baba mzazi wa Happiness, Joel Kaaya alimtelekeza yeye na mwanawe ambapo mpaka sasa haijulikani aliko.
Msuya alitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kusaidia hata ikiwezekana kumnunulia happiness kiti cha magurudumu kitakachorahisisha kumpeleka Hospitali na hata kutoka nje kucheza na wasichana wenzie.Pia siku hiyo, Siti alitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu, Nassoro Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kununu vipuri vya kutengenezea baiskeli yake.