MSIBA
Na.Mwandishi wetu.
Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma
kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao
kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika
simu yake wakati akitembea kwenye reli.
Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia
kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.
Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer
Inter-School concert iliyoandaliwa na group ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia
alishinda dougie competition wakati
5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.
Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri
mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani,
Amen.