MOTO MKUBWA IRINGA
Polisi wakiweka doria katika eneo la tukio wakati maduka yalipoteketea kwa mto mkoani Iringa usiku wa kuamkia leo.
Moto
mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza zaidi maduka 10
eneo la Miyomboni katika Manispaa ya Iringa usiku huu.
Moto
huo ambao chanzo chake bado kufahamika umezuka majira ya saa 2 usiku wa
kuamkia leo katika eneo hilo la Uhindini kata ya Miyomboni mjini Iringa.
Baadhi
ya wafanyabiashara waliokumbwa na tukio hilo la moto kuteketeza maduka
yaowamesema kuwa moto
huo ulianza katika chumba kimoja wapo cha duka na kuwa wanahisi ni
hitirafu ya umeme.
Hata
hivyo wamesema kuwa baada ya moto huo kuanza kuwaka walipata
ushirikiano kutoka kwa kikosi cha zima moto Manispaa ya Iringa ambao
walifika kwa wakati na kuishiwa maji kabla ya kuuzima moto huo.
Pia
walisema wakati gari la zima moto limekwenda kuchota maji mto Ruaha
vibaka walitumia nafasi hiyo kupora mali mbali mbali na kujikuta
wakiishia katika mikono ya polisi ambao walitanda eneo hilo.
Diwani
wa kata ya Miyombini kitanzini Jesca Msambatavangu amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo pamoja na kukipongeza kikosi cha Zimamoto mjini
Iringa kwa kufika kwa wakati eneo la tukio huku akiwataka wananchi
kuacha kulaumu kikosi hicho kwa kazi kubwa waliyoifanya.