MOJA YA KANISA LILILO CHOMWA JUZI ZANZAIBAR


(Moja ya makanisa yaliyochomwa Zanzibar hivi karibuni)
Ndugu zangu,
Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi  binafsi na ya kundi dogo  badala ya yale ya  kitaifa.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao. Kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania.
 Mungu Ibariki Tanzania.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)