MKUU WA WILAYA YA KATAVI ATAKA USHIRIKIANO
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Tusamale Mwamlima amewataka watendaji
wa serikali katika halmashauri ya Mji na wilaya ya Mpanda katika
wilaya anayoongoza kumpatia ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi
katika utumishi wa umma ili kuwaletea wananchi maendeleo ambayo ndiyo
wanayoyatengemea na kuachana mamalamiko kama watendaji wao.
Changamoto hiyo ameitoa leo wakati akiongea na watendaji wa
halmashauri hizo alizitembelea ofisi ni kujitambulisha na kufahamiana
tangu kuteuliwa na Mh.Rais Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya hiyo
kufuatia aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyoDr Rajabu Rutengwe kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Mkuu huyo wa wilaya almesema hakuna mtu yeyote anayefanikiwa bila
kuwa na ushirikiano wa karibu bila ushirikiano hakuna mafanikio,hivyo
anaomba ushirikiano wa karibu kwa watendaji na wananchi kwa ujumla.
Katika kikao hivyo mkuu huyo wa wilaya ametaja mambo matano
yaliyoko mbele yao kwa ajili kuhakikisha yanatekelezwa ili kufanikisha
maendeleo kwa wananchi ,moja ya mambo hayo ni uwepo amani ili
kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika augost 26
mwaka huu,
Jambo la pili maazimisho ya sherehe za wakulima nanenane ambapo
tunatakiwa kufanya vizuri ili kuweza kutunza ushindi uliopatikana mwaka
wa jana katika maazimisho hayo ambapo wilaya ya mpanda iliibuka mshindi
wa kwanza kikanda kwa kanda ya nyanda za ju kusini katika halmashauri
za mikoa ya nyanda za juu kusini ambazo ni Mbeya, Rukwa,
Ruvuma,Iringa,Katavi na Njombe.
Jambo lingine alilosisitiza kuhusu mbio za mwenge pamoja na
maandalizi ya mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya,na kuwataka watu wa
vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha watu wanakuwa huru kutoa maoni
yao kuhusu mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya katika tume ya kukusanya
maoni inayoongozwa na jaji Joseph walioba itakapotembelea mikoa
kukusanya maoni watu wajitokeze kutoa maoni yao.
Kwa upandewake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilayaa ya
Mpanda Justin Tibenderana alitoa taarifa fupi kwa mkuu huyo wa wilaya
kwa kueleza hali ya wilaya na shughuli za maendeleo,hali ya kiutawala,
na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwa ni
pamoja na shughuli za kilimo cha mazao ya biashara ambapo wanategemea
zao la tumbaku na kahawa kwa kiasi kidogo,
Amesema kuwa kwa sasa wilaya imeazisha zao la kilimo cha miembe ili
liwe zao la biashara ambalo litakuwa zao mbadala ya zao la tumbaku
ambalo lianharibu mazingira.