MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MATIBABU YA FISTULA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania ,katika viwanja vya Mnazi mmoja Juni 15,2012. (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dk, Wilbroud Slaa. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi  wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania ,Juni 15 2012 katika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar eSalaam , Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete,(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Baadhi ya wagojwa waliotibiwa FISTULA wakiimba na kutoka ushuhuda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula Tanzania ,Juni 15,2012 jijini Dar es Salaam, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye miwani ) akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa  Kampeni ya Matibabu ya Fistula Tanzania Juni 15-2012 jijini Dar es Salaam, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dk. Wilbroud Slaa,(kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa DSM ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA Beatrice Mlunga (kulia) akitoa ushuhuda wa matatizo alliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula Tanzania katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam ,Juni 15,2012. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kuacha kujificha  kwani ugonjwa huo unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana bure katika hospitali ya  CCBRT jijini Dar es salaam na Hospitali ya Kanisa la ya Kilutheli ya Selian kushoto ni mume wa shuhuda huyo Hosea Sanga, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA