MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012 KUMEKUCHA
Wadhamini wakuu wa shindano hilo la Miss Utalii Kanda ya ziwa 2012 ni kampuni ya Gold Master, huku wadhamini wengine wakiwa ni hoteli ya kitalii ya Monarch Hotel ya mjini Mwanza, magazeti ya Jamboleo.
Warembo wote wameanza kambi ya mazoezi katika hoteli hiyo ya Monarch Hotel Mwanza, wakiwa chini ya ukufunzi wa Rose Mary Kasiga Miss Utalii Mwanza 2011 na Fania Hassani Miss Utalii Dodoma 2007.
Aidha waandaaji wameomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ,ambalo ni la pekee na lenye manufaa makubwa kiuchumi na kitamaduni kwa kanda ya ziwa na taifa kwa ujumla, kwani tofauti na mashindano mengine Miss Utalii tanzania linalenga kutangaza na kuhamasisha utalii,utamduni,mianya ya uwekezaji,elimu,afya ya jamii,maliasili za taifa,mazingira,bidhaa za Tanzania na vita dhidi ya uwindaji haramu,uvuvi haramu n, mila kongwe na potofu.
Washindi wa shindano hilo watawakilisha mikoa ya kanda ya Ziwa katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012,ZITAKAZO FANYIKA NOVEMBA 2012