MAONYESHO YA TANZANIA HOMES EXPO YALIVYO FANYIKA JANA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuph Mwenda (katikati) akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya wadau wa kukopesha nyumba
(Tanzania Homes Expo) kupitia benki mbalimbali nchini ambapo wananchi
wanaonyeshwa urahisi wa kuweza kukopa nyumba maonyesho hayo yamefanyika
leo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam Kushoto ni
Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw. Zenno
Ngowi.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuph Mwenda, akipewa maelezo
katika banda la Benki ya Akiba Commercial wakati akitembelea Kampuni
zilizoshiriki katika maonyesho hayo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuph Mwenda, akikagua baadhi ya
makabrasha katika banda la Shirika la nyumba Tanzania NHC kushoto ni
Afisa masoko wa Shirika hilo na mmiliki wa blogu ya mitindo ya Misspopular Mariam Iddi na kulia ni Afisa mauzo
mwandamizi wa shirika la nyumba Tanzania (NHC) Bw. Emanuel Lymo.
Meya wa manispaa ya Kinondoni Mhe. Yusuph Mwenda (kulia) akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana na maonyesho hayo na kushoto ni
Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw. Zenno Ngowi.
Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw. Zenno
Ngowi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya maonyesho hayo
ambapo alisema huo ni mwanzo tu na wanatarajia kuendelea kuonyesha kwa
miaka mingine ijayo.