Skip to main content
Mamilioni ya Wamisri wakusanyika Cairo katika Medani ya Tahrir
Mamilioni
ya wananchi wa Misri hii leo wameendelea kukukusanyika katika Medani ya
Tahrir mjini Cairo baada ya Swala ya Ijumaa, kulalamikia hatua ya
Baraza la Kijeshi linaotawala nchini humo ya kung'ang'ania madaraka.
Wananchi hao pia wanalalamikia hatua ya wanajeshi hao ya kuchelewesha
kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni. Aidha
Wamisri wamelaani kupunguzwa uwezo wa rais wa nchi na uwezekano wa
wanajeshi hao kufanya mapinduzi dhidi ya mwenendo mzima wa demokrasia
nchini humo.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, Baraza la Kijeshi
la Misri (SCAF) limesema kwamba litatumia vikosi vya jeshi dhidi ya
waandamanaji ambao wamejikusanya katika Medani ya Tahrir kwa madai ya
kulinda maslahi ya taifa. Aidha baraza hilo limeikosoa harakati ya
Ikhwanul Muslimin eti kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais mapema
na kudai kuwa kutangaza matokeo hayo yasiyo rasmi kumesababisha
mgawanyiko na vurugu nchini Misri.