MABONDIA WA TANZANIA WAWEKWA KWENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani
(IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika orodha ya viwango .
Francis Miyeyusho, Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal Bruno na Francis Cheka.
Katika kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings Committee) ambacho kilikaa
jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA iliridhishwa na
viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa watawaangalia
kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili kuwaongeza
katika orodha ya viwango.
Hii ina maana kuwa mabondia hao waliowekwa kwenye orodha ya viwango
vya IBF vya mabara wanaweza kupigania ubingwa wa IBF wa Afrika na
mabara wakati wowote.
Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi iliwakilishwa kwenye
kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka Tanzania. Katika vikao hivi
vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu wa IBF wanaohudhuria
peke yao.
Ngowi aliwapendekeza pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika
ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana,
Nigeria, Morocco, Cameroon, Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na
Jordan.
Kumekuwepo na uchakachuaji mkubwa wa rekodi za mabondia katika bara la
Afrika kwa mapromota na mawakala wa ngumi kuweka viwango vya mapambano
ya uongo katika rekodi za mabondia wao kweney mtandao wa Boxrec. Hii
inawapa wakati mgumi sana mabondia wa Kiafrika kupata mapambano ya
ngumi ya kimataifa.
Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi inaongozwa na rais wake Onesmo Ngowi wa Tanzania.