EURO 2012 STATS TO DAY
VIKOSI VYA LEO |
POLAND Szczesny Piszczek, Wasilewski, Perquis, Boenisch Murawski, Polanski Blaszczykowski, Obraniak, Rybus Lewandowski |
UGIRIKI
Chalkias Torosidis, P'thopoulos, P'dopoulos, Holebas Karagounis, Katsouranis, ManiatisSalpingidis, Gekas, Samaras |
WENYEJI washirika wa Euro wa 2012, Poland hawana majeruhi kuelekea mechi yao ya ufunguzi wa michuano hiyo na kocha Franciszek Smuda anatarajiwa kushusha kikosi kile kile kilichocheza mechi mbili zilizopita za kirafiki.
Hiyo inamaanisha, wachezaji wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek, Jakob Blaszczykowski na Robert Lewandowski wataanza, wakati Rafal Murawski na Eugen Polanski watasimama katika safu ya kiungo wakati 'Tai Mweupe' akifungua kampeni za michuano hiyo.
Ugiriki nao wapo kamili na leo wanatarajiwa kutumia mfumo wa 4-3-3 dhidi ya wenyeji hao. Vasilis Torosidis yuko shakani kucheza kufuatia kuumia goti dhidi ya Slovenia wiki iliyopita, lakini beki huyo wa kulia amekuwa akifanya mazoezi siku za karibuni.
Sotiris Ninis pia ni majeruhi,licha ya kinda huyon wa miaka 21 kuelezwa kwamba yuko fiti na atacheza. Mshambuliaji huyo wa Panathinaikos, anaweza kuanzia kwenye benchi katika mechi ya leo na Dimitris Salpingidis anatarajiwa kucheza upande wa kulia katika safu ya washambuliaji watatu.