DULLY SYKES AOMBA MSAMAHA
Msanii maarufu wa bongo fleva Dully Sykes amewaomba msamaha mashabiki
wake kwa kauli aliyoitoa jana katika kipindi cha XXL kinachorushwa na
Clouds fm. Akiongea katika kipindi cha ampifaya Dully amesema sababu
iliyomfanya atoe kauli ile ni hasira alizokua nazo wakati anapigiwa simu
na Sudy Brown. Dully Sykes jana katika kipindi cha XXL kupitia segment
yake ya you heard inayosimamiwa na Gossip cop Sudy Brown,
Sudy alimpigia simu Dully kutaka kujua suala la nyimbo ya Mwana FA
inayokwenda kwa jina la amen ambayo dully amepewa shavu, nyimbo hiyo
inasemekana imekopiwa kutoka kwenye nyimbo ya cecile wa Jamaica. Baada
ya kupigiwa simu dully alitoa kauli zilizotafsiriwa kama ni matusi.
Lakini kwa kuonesha kutambua kosa lake dully ameomba msamaha mashabiki wake.