Bingwa wa
Dunia wa uzani wa welter tawi la masumbwi la WBO Manny Pacquiao
amepoteza taji lake kwa mara ya kwanza aliposhindwa na Mmarekani Timothy
Bradley kufuatia uwamuzi wa kutatanisha mjini Las Vegas.
Licha
ya Pacquiao kupiga ngumi 94 ikiwa ni zaidi ya mpinzani kiwango cha
kwake, Mfilipino huyo alishindwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
miaka saba baada ya waamuzi wawili kuamua kuwa Timothy Bradley ameshinda
kwa 115-113, uwamuzi uliegemea hilo.
Mwamuzi mwingine alitofautiana na wenzake akimpa ushindi Pacquiao wa 115-113.
Watazamaji
wa pambano hilo hawakuridhika na uwamuzi uliotangazwa na walizomea sana
baada ya Bradley kutangazwa kua mshindi na hilo limezua uwezekano wa
pambano la marudio baadaye mwaka huu.
"nilihisi
nimeshinda," alisema Bradley, ambaye hapo kabla alikua amechapisha
tiketi kabambe za kuonyesha pambano la marudano kufanyika tarehe 10
novemba.
Bradley aliongezea kusema kua "sidhani ni hodari kama wengi walivyomsifu. Makonde yake hayakua na nguvu."
Pacquiao
alichelewa kuingia ukumbini lakini alipoingia alianza raundi ya kwanza
kiuzembe uzembe ingawa alirusha ngumi tatu katika sekundi za mwisho wa
raundi.
Hadi
kufikia raundi ya tano Bradley alionekana kuzidiwa kutokana na maumivu
ya jeraha la kidole cha mguu ikionekana kua Pacquiao anaelekea kupata
ushindi wa mteremko.
Manny Pacquiao
Kwa upande wa Bradley alifanya vizuri katika raundi tatu za mwisho lakini watazamaji hawakuridhika na hilo.
Promota
wa masumbwi, Bob Bradley alisema haiaminiki. Aliongezea kusema kua
punde baada ya pambano kumalizika, alikwenda kwake Bradley na
akamwambia, Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu lakini sikuweza kumshinda
mtu huyo.'"
Pacquiao mwenyewe alisema hakuweza kuamini matokeo hayo. Aliongezea kua nimejitahidi lakini naona juhudi zangu hazikutosha.
Ngumi zake hazikunidhuru, mara nyingi ngumi zake ziliishia kwenye mikono yangu.alisema Pacquiao.