ASUBUHI YA LEO MNH
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari, ambaye anaongoza mgomo wa madaktari nchini Dk.Steven Ulimboka akiwa
na majeraha baada ya kutekwa na kushambuliwa na watu wasio julikana na kutupwa
msitu wa Mabwe Pande uliopo nje ya jiji la Dar es Salaam usiku wa kuakia
leo.
Dk. Cathbert Mchalo wa Taasisi ya Mifupa ya Moi
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumpokea, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari Tanzania kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha
aliyopata kutokana na kipigo.
Ofisa wa Polisi akimzuia mpiga picha wa gazeti
la Tanzania Daima, Francis Dande, asimpige picha wakati wakimuondoa askari
mwenzao aliyeshambuliwa na madaktari akituhumiwa kukutwa akipiga simu ya
kuwataarifu wenzake kuwa Dk. Ulimboka hakufa.
Mmoja wa wana usalama wa (wa pili ushoto),
akizozana na madaktari baada ya kumbaini akijifanya ni mwandishi wa habari na
kumuamuru kuondoka eneo hilo mara moja.
Mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), wa pili kulia, akizozana na Askari Polisi waliofika hospitalini
hapo wakidai wanatafuta redio yao ya mawasiliano iliyopotea wakati wa
pilikapilika za kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa
madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, alipoletwa akiwa hoi kutokana na kipigo
kutoka kwa watu waliomteka usiku wa kuamkia jana na kumtupa msitu wa
Mabwepande.
Madaktari wakiwa wamepigwa butwaa nje ya viwanja
vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia tukio hilo.
![]() |
|
Wauguzi wakiwa nje ya wodi ya Kibasila
wakitafakari jambo kufuatia jambo hilo