30 WAINGIA KWENYE KOZI YA KUJENGA AFYA

Walimu
18 wa shule za msingi na makocha 12 wa mpira wa miguu wanashiriki kozi
ya mpango maalumu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa miguu.
Kozi
hiyo ya siku tano inayoitwa FIFA 11 for Health imeanza leo (Juni 11
mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na itamalizika Juni 15 mwaka huu.
Mafunzo
hayo yanaendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ambapo ujumbe katika 11 for
Health ni 1. Cheza mpira, 2. heshimu wasichana na wanawake, 3. jikinge
na virusi vya Ukimwi (HIV), 4. epuka dawa za kulevya, pombe na sigara,
5. tumia neti zenye viuatilifu, 6. nawa mikono yako, 7. kunywa maji
salama, 8. kula chakula chenye mpangilio, 9. pata chanjo, 10. tumia dawa
sahihi na 11. cheza mchezo mzuri.
Walimu
hao kutoka shule za Mkoa wa Dar es Salaam ni Aloyce Rutta (Montfort,
Temeke), David Kazinge (Temeke, Temeke), Rajabu Ased (Mtoni Kijichi,
Temeke), Mathew Kambona (Mji Mwema, Temeke), Ruth Mahenge (Chang’ombe,
Temeke), Abdul Mikoroti (Nzasa, Temeke), Exuperus Kisaka (Mavurunza,
Ilala), Khadija Kambi (Karume, Ilala) na Hamisi Ibrahim (Tusiime,
Ilala).
Wengine
ni Baltazar Kagimbo (Tabata Jica, Ilala), Isaac Mhanza (Airwing,
Ilala), Baraka Baltazar (Muhimbili, Ilala), Job Ndugusa (Upanga, Ilala),
Tumaini Hiluka (Buguruni, Ilala), Maua Rashid (Uhuru Wasichana, Ilala),
Mussa Kapama (Bunju A, Kinondoni), Raymond Rupia (St. Anne Maria,
Kinondoni) na Priscus Shilayo (JK Nyerere, Kinondoni).
Kwa
upande wa makocha ni Dismas Haonga, Frank Mwakang’ata, John Sebabili,
Michael Bundala, Peter Manyika, Raphael Matola, Renatus Magolanga,
Robert Mayunga, Said Pambaleo, Seba Nkoma Titus Michael na Wilfred
Kidao.
Programu
hiyo inalenga watoto ambapo washiriki watakaofaulu katika kozi hiyo
ndiyo baadaye watakuwa wakufunzi kwa ajili ya kuifanya katika maeneo
mbalimbali nchini.