TFF IKO MBIONI KUJIUNGA NA SUPER SPORT

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, liko katika mchakato wa mazungumzo na kituo cha SuperSport cha Afrika Kusini kwa ajili ya kuonyesha mechi zake za Ligi Kuu msimu ujao.

Wakati TFF ikijipanga kufanya hivyo, kituo hicho tayari kinafanya hivyo kwa Ligi Kuu ya Kenya na Uganda.

Itakumbukwa, Super Sport ilikuwa ikionyesha baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara na zaidi ni zile zinazohusisha timu za Simba na Yanga na kuonekana sehemu mbalimbali duniani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Walas Karia alisema katika mazungumzo ya kwanza pande hizo mbili zilishindwa kufikia makubaliano na baada ya Super Sport kutoa  kupendekeza yake kuwa baadhi ya mambo lazima yafanyike iweze kudhamini ligi hiyo.

"Kwa sasa kamati ipo katika harakati kukutana na viongozi wa Super Sport kuhakikisha Ligi Kuu msimu ujao inakuwa ya kuvutia ikiwemo pia kutafuta wadhamini mbalimbali lengo likiwa kupunguza makali ya gharama za uendeshaji kwa klabu."

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)