NYARAKA ZA PAPA SIRI ZAVUJA

Nyaraka hizo zinashutumu vitendo vya rushwa na kushindania madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican amesema hii ni kashfa kubwa kuliko zote dhidi ya Papa Benedict tangu apate wadhifa wake huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua Kanisa Katoliki nyakati hizi.
Mhudumu mkuu wa Papa, Paolo Gabriele, amekamatwa na tume ya Vatican inachunguza watu wengine ambao wamehusika katika kashfa hiyo