Nizar Khalfani




KIPA Mghana, Yaw Berko, amesaini mkataba mpya na Yanga huku kiungo, Nizar Khalfan, naye akimwaga wino Jangwani kuitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mbali na hao, Mwanaspoti linajua kwamba Yanga imefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi, lakini bado hajasaini mkataba wowote.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya Yanga, zinasema kuwa Nizar alisaini Yanga hata kabla ya kufanya mazungumzo na Simba ambayo ilitaka kumtambulisha hivi karibuni.

Mmoja watendaji wakubwa wa kamati hiyo alidokeza pia kuwa wametega rada kuwanasa beki wa kulia wa Mtibwa Sugar, Juma Abdul na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Danny Mrwanda.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiongozi huyo alidai klabu hiyo inataka kufanya usajili imara kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya Kagame.

"Kama unavyojua tumefanya vibaya sana msimu uliopita, ni jambo la kusikitisha bingwa mtetezi anaanguka hadi nafasi ya tatu, hicho kitu kimetuuma na hatutaki kijirudie," alisema kiongozi huyo.

"Sasa hivi tutakuwa makini sana kwenye usajili kuhakikisha kwamba tunasajili wachezaji wenye viwango na watakaoisaidia timu hii.

"Hatutaki kuchukua tena wachezaji bomu, kila nafasi uwanjani tunataka iwe na mtu wa uhakika."
Alisema Nizar tayari ameshasaini Yanga na Bahanuzi wamezungumza naye.

"Sasa hivi tuko katika mchakato wa kuwanasa Juma Abdul yule beki wa pembeni wa Mtibwa, tunaamini atatusaidia sana kwani ukiangalia umri wa Shadrack Nsajigwa nao umekwenda hivyo tunataka kusajili damu changa ili asaidiane nao," aliongeza.

"Pia Mrwanda naye yuko katika rada zetu kwani tunaamini ni mshambuliaji mzuri hivyo hapa tunamshawishi aweze kujiunga na sisi na naamini atakubali kutokana na fedha tutakayompa."

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA