Jumapili hii kulikuwa na bonanza la mchezo wa mpira wa miguu hapa Arusha ambapo timu ya Arusha Wazee Sports Club iliialika timu ya Bunge la Kenya kwenye mchezo wa kirafiki. Timu nyingine mbili za Bunge la Afrika Mashariki na TGT Arusha zilishiriki bonanza hilo ambapo timu ya Arusha Wazee iliibuka kidedea na kujinyakulia kombe baada ya kuwafunga Wabunge wa Kenya 5-3 kwa mikwaju ya penalt. Baada ya hapo kukafanyika tafrija kubwa ya msosi na vinywaji pamoja na muziki uwanjani hapohapo. Shukrani ziwaendee Bunge la Afrika Mashariki, TBL na Tanzania Distilleries Ltd walioshirikiana na Wazee kufadhili bonanza hilo, Bunge la Kenya sasa limeialika timu ya Wazee Arusha kwenda Mombasa kwa ziara ya kirafiki ya kimichezo mwishoni mwa mwezi wa Agosti wakati wa Mombasa Agricultural Show ili kuimrisha ushirikiano ndano ya Jumiya ya Afrika Mashariki.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA